Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amefanya Ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya Maendeleo katika shule ya Msingi Kakuni, Kibaoni, Kavuu, na shule ya Sekondari Ikuba pamoja na kuona ukamilishaji wa Daraja la Msadya katika Wilaya ya Mlele Halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.
Katika ziara hiyo mhe. Mrindoko amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto kuripoti shule katika shule za msingi kwa wanaoanza darasa la awali na Sekondari kwa kidato cha kwanza ili waweze kuanza masomo kwa wakati
Aidha amewataka walimu , wazazi, na wanafunzi kuendelea kutunza madarasa ambayo yanajengwa na Serikali ili yasiweze kuharibika haraka.
Pia amewapongeza wananchi kwa kuendelea kutoa maeneo ambayo miradi ya maendeleo inajengwa katika maeneo yao hali inayo onesha muitikio mkubwa kwa wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande wake Clesensia Joseph ambaye ni kaimu RASI katika mkoa wa katavi amewataka wazazi na walezi kuepuka mila potofu ambazo zina mkosesha mtoto kupata haki yake ya elimu ikiwemo za ndoa za utotoni maarufu Chagulaga.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa