Wakulima katika Halmashauri ya Mpimbwe wameaswa kutumia mbolea ya Ruzuku ilikuweza kuongeza kiwango cha mazao katika uzalishaji .
Akiongea na wananchi wa Mpimbwe katika mkutano wa hadhara Afisa Kilimo Odetha Kijika amesema baadhi ya wamiliki wa Mashamba wamekuwa wakikataa kutumia mbolea kwa madai kuwa mbolea husababisha ardhi kupoteza Rutuba jambo ambalo sikweli.
Amesema Ardhi ya Mpimbwe imebadilika sasa tofauti na zamani kwani hivi sasa mbolea inahitajika kutokana na Aridhi kuchoka kwa kutumika kwa mdamrefu hivyo kulazimika kutumia mbolea.
Hivyo amewataka wananchi kuendelea kutumia mbolea za ruzuku ili kuepuka kukosa mazao na kusababisha hali ya ukosefu wa chakula na kipato katika familia.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa