Uharibifu wa miundombinu ya njia za maji zimesababisha kijiji cha Iziwasungu kata ya Kasansa Halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi kukumbwa na mafuriko na baadhi ya wananchi nyumba zao kubomoka na kupelekea kukosa maeneo ya kuishi na wengine nyumba zao kuingiliwa na maji.
Mkuu wa wilaya ya Mlele Mhe. Majid Mwanga , Mwenyekiti wa Halmashauri Silas Ilumba ,Mkurugenzi Mtendaji Bi. Catherine Mashall pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama Wamefika katika Kijiji cha Iziwasungu kutoa pole kwa Waathirika hao.
Mkuu wa Wilaya wa Mlele Mhe Majid Mwanga amewataka wananchi kuendelea kuchukua Tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa kuchemsha maji ya kunywa na kuhakikisha wanawalinda watoto ilikuweza kuepusha ajali za watoto kutumbukia kwenye maji.
Aidha amesema kutokana na mafuriko hayo aliyotokea Usiku wa Tarehe 12 Mwezi 4 mwaka 2023 Kaya takribani 12 zimeathirika kwa kukosa Makazi ambapo jitihada za awali zimechukuliwa na kuwapatia Turubai za kulalia na kuwataka kulala shuleni wakati wakisubiri maji yapungue .
Aidha amewataka walio sababisha uharibifu huo kufikia Tarehe 17 mwezi huu
Wawe wameweka mipango thabiti ya namna ya kuyaruhusu maji hayo kupita katika njia yake ya zamani kabla sheria haijachukuliwa dhidi yao.
Akieleza chanzo cha Mafuriko Hayo Mwenyekiti wa Halmashauri Silas Ilumba Amesema Baadhi ya wananchi walichepusha maji kutoka mtoni na kupeleka katika Mbuga za mpunga hali iliyosababisha Mto kuacha njia yake na kuingia katika maeneo ya wananchi.
Akitoa mwarobaini wa tatizo hilo Matrida Juakali ambaye ni mwathirika wa mafuriko hayo amesema njia sahihi ya kupata suluhu nikuhakikisha mto unarudishwa katika njia yake ilikuweza kunusuru kaya hizo.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa