Asasi isiyo ya kiserikali UDESO (Usevya Development Society) iliyopo halmasahuri ya wilaya ya Mpimbwe mkoa wa Katavi, siku ya jumatano tarehe 28 Agosti 2024 imefanya wasilisho la mradi wa NINAWAJIBIKA. Walioshiriki katika kikao hicho cha uwasilishaji ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mlele Mhe. Majid Mwanga, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe Bi Shamim Mwariko na wadau mbalimbali.
Akiongea mratibu wa UDESO Paul Jackob Masanja amesema mradi wa ninawajibika utatekelezwa Tanzania bara katika mikoa 15, ndani ya halmasahuri 15 na kila halmashauri mradi utafikia vijiji vitatu chini ya shirika linalofanya kazi katika halmasahuri hiyo ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe mradi utafanyika kata ya Kibaoni katika vijiji vya Kibaoni, Ilalanguru na Mirumba
Masanja ameongeza kuwa, imeonakana bado kuna udhaifu katika usimamizi wa fedha za umma, hivyo mradi umelenga kuwapa elimu wananchi na wadau mabalimbali wa maendeleo katika kujua mapato na matumizi ya fedha, kujua thamani ya miradi, kufahamu ubora wa miradi na gharama zilizotumika na kupata uwazi juu ya mikataba ya manunuzi.
Nae mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Mpimbwe Bi Shamimu Mwariko amewapongeza UDESO kwa kuwa msatari wa mbele kuchangia maendeleo kwa kupititia miradi mbalimbali na kuwaahidi kwamba atashirikiana nao, pia aliwaasa kwamba ni vizuri kutoa taarifa mapema ili wapewe takwimu iliyoandaliwa kwa usahihi na kuhakikisha wanashirikisha watu wenye nia njema na serikali sio waliopo kwa ajili ya masalahi binafsi.
Mkuu wa wilaya ya Mlele pia amewasihi UDESO wasiingize siasa katika taasisi yao bali watoe elimu nzuri kwa wananchi bila upendeleo na amewashauri kukitumia chombo cha habari cha halmashuri ya Mpimbwe, Mpimbwe fm radio ili kufikisha elimu kwa watu wengi kwa haraka bila kutumia gharama kubwa.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa