Leo tarehe 11 Oktoba 2024, Bi. Shamim Mwarikon, msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, amezindua rasmi zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Shule ya Sekondari Usevya. Kituo hiki, kilichopo Kata ya Usevya, Kitongoji cha Kaunyala, kinategemewa kuwa kimbilio la wananchi waliokuwa wakisubiri kwa hamu zoezi hili muhimu. Bi. Shamim amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanapata haki ya kushiriki uchaguzi, akisisitiza kuwa uandikishaji huu wa siku 10 ni fursa muhimu kwa kila mmoja. Zoezi hili litakamilika tarehe 20 Oktoba 2024.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa