Wadau wa Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoa wa katavi wamekutana kujadili hali ya utekeleza wa elimu kuanzia 2019 hadi mwezi April 2022 katika ukumbi wa shule ya sekondari Usevya.
Wakijadili kuhusu hali ya ya ufaulu wa wanafunzi wamesema Halmashauri ya wilaya ya Mpimnbwe ina Tarafa mbili ambazo ni Tarafa ya Mamba na Tarafa ya Mpimbwe pia ina kata 9 Ambazo ni Kibaoni , Usevya, Ikuba, Chamalendi , Mwamapuli, Mbede, Majimpoto Mamba ,na Kasansa Halmashauri hiyo ina jumla ya shule za msingi 42 na 8 za sekondari shule hizo zimesajiliwa na zina milikiwa na Serikali .
Akisoma Taarifa ya hali ya Maendeleo ya Elimu kwa mwaka 2019 hadi april 2022 Florence Ngua Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa katavi amesema katika ufaulu wa mitihani darasa la saba 2021 Halmashauri ilishika nafasi ya tatu kimkoa kwa asilimia ya ufaulu wa 89.7% kwa mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kupongwezwa
katika matokeo ya ufaulu katika Elimu Sekondari kwa mwaka 2018,2019,2020 na 2021 hali ya ufaulu wa mitihani iliongezeka kitaifa kidato cha nne kwa 11.4% kwa mwaka 2018 ufaulu ulikuwa 86.1% ,mwaka 2020 ni 97.53% na kwa mwaka 2021 ni 99%.
Kidato cha pili mwaka 2018 ufaulu ulukuwa asilimia 92.96% ,mwaka 2020 ufaulu uliongezeka kwa asilimia 92.98%na mwaka 2021 ufaulu ulikuwa 95% na kwa kidato cha sita mwaka 2018 ufauLu ulikuwa 100% na mwaka 2021 ni 99%
Aidha Florence ameeleza juu ya changamoto zinazoikabili idara ya elimu na namna ambavyo wanapambana ukabiliana nazo , amesema kumekuwa na changamoto za upungufu wa nyumba za walimu, vyumba vya madarasa, na hosteli kwa sekondari upungufu wa samani hususani madawati kwa shule za msingi kutokana kwa na sera ya Elimu bila malipo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanao andikishwa , ufinyu wa Bajeti ya Elimu unaosababisha Idara kutofikia malengo yake kwa ufanisi na kwa wakati , utoro wa rejareja kwa baadhi ya wanafunzi unachangia kwa kiasikikubwa kutokuwa na ufaulu mzuri ,ukosefu wa walimu wa sayansi , hisabati , kiingereza na mafundi sanifu wa maabara kwa shule za sekondari.
pia ameeleza namna amabvyo wanapambana katika kukabiliana na changamoto hizi ikiwa ni pamoja na kuendelea kuomba ofisi ya Rais TAMISEMI kuongezewa Walimu , kutengeneza viti , meza na madawati na nakufaya ukarabati pale vinapoharbika ,kuongeza ujenzi wa shule mpya za msingi na Sekondari pia wakuu wa shule Bodi za shule , walimu na kamati za shule kushirikiana na wazazi na wadau wa elimu kuendelea kudhibiti utoro .
Sanjari na hayo wadau wameshauri juu ya kuwajali walimu kwa kuwaaamini kwakuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuhakikisha watoto wanakuwa na elimu bora
Hata hivyo Mgeni rasmi katika kikao hiki Dr Elpidius Baganda katibu tawala msaidizi Elimu amesema wazazi pamoja nwa dawau wengine washirikiane katika kukuza elimu kwa kutoa mahitaji yote muhimu kwa mwanafunzi .
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa