Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kata ya Usevya imeazimisha siku ya Wanawake tarehe 26/2/2024 ikiwa ni ngazi ya Kata. Mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo alikua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Bi Shamim Mwariko.
Katika sherehe hiyo yenye kauli mbiu “Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii ” mgeni rasmi aliwahutubia wanawake na kuwataka kueleza kero na changamoto wanazokumbana nazo kwenye familia zao na wakiwa kwenye harakati za kujitafutia kipato chao cha kila siku.
Wanawake walifunguka na kusema wanahitaji serikali ya awamu ya sita kuwapatia mikopo ili waweze kuendesha bishara zao.
Pia ukatili kwa wanawake imekua ni changamoto kubwa, wanawake wanapigwa wananyanyaswa kijinsia na kupelekea kukatisha ndoto zao.
Mkurugenzi Mtendaji alihitimisha kwa kusema, wanawake tupendane sisi kwa sisi, pia tusiogope kupaza sauti juu ya vitendo vya kikatili tunavyofanyiwa.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa