Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amesema moja ya mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo kwanza ni kuhakikisha chanjo zinakuwa za kutosha, kusambaza magari kila kata na wataalamu watakaofanya kazi ya kutoa elimu na kutoa chanjo na kwa ambao tayari wameadhirika na ugonjwa huo wapate tiba.
Amesema hayo Akiwa katika mkutano na Wananchi wa kata ya Majimoto katika kitongoji cha Bula katika Halmashauri ya Mpimbwe.
DC Mwanga amewaonya waganga wa tiba mbadala kuwarubuni wananchi kuwa wanatibu ugonjwa huo kwani Serikali haitasita kumchukulia hatua mganga yoyote atakayebainika kumtubia mtoto kwa njia ya tiba mbadala.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuachana na imani potofu kuwa vifo vinavyotokea vinasababishwa na inamani za kishirikina bali wasikilize maelekezo ya madokta kwa kuwapeleka watoto wao wenye umri wa kuanzia miezi 4 hadi miaka 5 kupata chanjo ya ugonjwa huo.
Kwa upandewake Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe Dkt.Martin lohay amesema vifo vitokanavyo na ugonjwa huo 12 na wagonjwa waliobainika hadi sasa 646
Dkt. Lohay amesema hadi sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa chanjo zakutosha hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano ilikukabiliana na Jambo hilo.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa