Katibu Tawala mkoa wa Katavi Hasan Mhe. Rugwa akiwa katika Halmashauri ya Mpimbwe amewataka wananchi kuendelea kutunza miti ili kuweza kuendelea kuhifadhi mazingira ambayo yatasaidia katika kuleta kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
"Zoezi hili la upandaji miti lina hatua nne ambazo zote kwa pamoja zikizingatiwa zitasaidia kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi, tuzingatie upandaji miti, ulinzi wa vyanzo vya maji, utunzaji wa miche ambayo inapandwa na usafi wa mazingira" Amesema Mhe. Rungwe
Katika hatua nyingine katibu Tawala wa mkoa wa Katavi Mhe. Rungwe amewataka wananchi wote kushiriki kikamilifu kwa kila familia kuhakikisha wanapanda Miti katika maeneo yao ya makazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Silas Ilumba amesema kutokana na kuwepo kwa wananchi wanao tumia sehemu za vyanzo vya Maji kufanya shughuli za kibinadamu, hali hiyo inasababisha vyanzo hivyo vya asili kukauka maji mapema, hivyo ametumia nafasi kumuomba mgeni rasmi, kutokana na ushirikiano uliopo kati ya mkoa wa Rukwa na Katavi kuweza kuliangalia swala hili ili kuepukana na uharibifu huo wa mazingira.
Naye Rajabu Ramadhan mratibu wa upandaji miti Mkoa wa Katavi amewataka kuendelea kusimamia upandaji na uendelezaji wa utunzaji wa miche hiyo iliyo pandwa ili kuweza kufikia malengo yaliyo kusudiwa.
Aidha Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Saka Muok amesema Halmashauri ya Mpimbwe inatarajia kupanda Miche 288,000 ambayo itapandwa katika shule za msingi, shule za sekondari, vituo vya Afya, zahanati, vijiji, na katika makazi ya watu binafsi.
Mwisho
*Imetolewa na:*
*Kitengo cha Mawasiliano Serikalini*
*Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe*
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa