Katibu tawala wa mkoa wa Katavi ndugu Albert Gabriel Msovela amewawakumbusha watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe kutambua majukumu yao na kuyatekeleza kwa weledi.
Ameyasema hayo siku ya Jumatatu ya tarehe 26 Agosti 2024 akiwa katika kikao cha ndani kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Usevya iliyopo kata ya Usevya halmasahuri ya (w) Mpimbwe kikao hicho kilihudhuriwa na baadhi ya viongozi kutoka mkoani Katavi, pia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mpimbwe Bi Shamimu Mwariko, wakuu wa idara zote za halmashauri ya Mpimbwe na watumishi wote kutoka sekta mbalimbali za halmashauri ya Mpimbwe.
Msovela amesema watumishi wote wanapaswa kutumia vizuri nafasi walizopewa ili kuwa na ufanisi wenye tija. Pia alisisitiza suala la nidhamu kazini na kuwaagiza maafisa utumishi kuhakikisha wanafuatilia uwajibikaji wa kila mtumishi aliyopo ndani ya halmashauri pia amesisitiza sana suala la upendo na ushirikiano kazini ili kazi zifanyike kwa wakati.
Aidha alikemea vikali kwa walimu wakuu wa shule za sekondari kwamba haitakiwi mwanafunzi yoyote wa kidato cha nne au cha sita kupata sifuri iwapo litatokea hilo basi mwalimu husika atawajibishwa.
Msovela alimalizia kwa kusisitiza kuwa elimu ya lishe iendelee kutolewa ili kuondoa udumavu kwa watoto wote mkoani Katavi hivyo mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe awe mstari wa mbele kusimamia suala hili kwa kushirikiana na watumishi wote wa sekta ya afya na wadau ili kuondokana na changamoto hiyo ya udumavu.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa