Mradi wa shule Bora umetoa mafunzo kwa Walimu wakuu , Waratibu Elimu kata , Maafisa Ustawi wa Jamii na watu wa Dawati la Jinsia leo katika shule ya Msingi Usevya
Mafunzo hayo yaliyobeba dhana nzima juu ya kupata namna bora ya kuhakikisha mwanafunzi anapata njia sahihi ya kufikisha Taarifa juu ya Ukatili wa kijinsia wanao fanyiwa katika jamii wanayoishi yalijikita hasa katika Maswala ya Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na Nje ya Shule, Uundaji na Uendeshaji Wa Mabaraza ya Watoto, Malezi, Unasihi na Ulinzi Wa Mtoto Shuleni,
Akifungua mafunzo hayo Afisa Elimu Mkoa Wa Katavi Bi. Upendo Rweyemamu amewataka kuhakikisha wanawapa Elimu yakutosha wanafunzi ilikuweza kutoa taarifa za Ukatili wanaofanyiwa kwa Walimu wa unasihi watakao chaguliwa na wanafunzi wenyewe
Pia amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya shule ilikuhakikisha Wanafunzi wanasoma kwenye mazingira Bora na rafiki lakini vitendo vya ukatili vinachochea kurudisha vyuma ufaulu wa wanafunzi vitendo ambavyo havitakiwi.
Aidha Bakari Geni Mratibu wa Shule Bora Mkoa wa Katavi amesema Njia salama zitakazo tumika kutoa taarifa kwa wanafunzi ni pamoja na kuwepo kwa sanduku la maoni ambapo funguo za sanduku hilo haliwezi kushikwa na mtu ambaye siyo Sahihi , ilikuepusha wanafunzi kuogopa kuweka maoni yao.
Kwa upande wao wanufaika wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia watoto kuwa na uwezo mkubwa wakujieleza pamoja na kuwa huru katika kutoa changamoto zinazo wakabili.
Mwisho.
Imetolewa na
Kitengo cha mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa