Na Odetha salumu. Mpimbwe ,Katavi
Akizungumza leo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Usevya Naibu waziri wa Sheria na Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mh.Geofrey Pinda amesema kikao hicho kina lenga kutambua changamoto zinazo wakabili watumishi ,kukumbushana majukumu ya utendaji kazi pamoja na kubadilishana mawazo kama familia moja .
Mh. Pinda amesema kuwa watumishi ndio chachu ya maendeleo katika jimbo kwani huchochea katika kukuza mapato ya Halmashauri kutokana na utendaji mzuri wakazi.
Mh. Pia amewataka watumishi hao kuazisha Saccos kwa ajili ya kuchangia Fedha ya pamoja na kuweza kukopeshana ilikujiinuilia kipato na kuanzisha shuguli mbalimbali za pamoja kupitia fedha walizonazo hivyo kuweza kuteua uongozi utakao simamia Saccos hiyo .
Aidha mesema kila mtumishi katika eneo lake anapaswa kufanya vikao vya wananchi pia kuhakikisha kila mtumishi anafahamu stahikizake ili kuweza kuiepukana na changamo wakati anapo staff, niwajibu wa Afisa utumishi kuweza kukutana na kutoa Elimu kwa watumishi ilikujua mtumishi anapaswa awe na vitu gani vitavyo msaidia kipindi atakapo staff.
Sanjali na hayo Naibu Waziri amewaambia watumishi kuangalia mahali patakapo tengenezwa uwanja kwa ajili ya kuinua vipaji vya Watoto kwani michezo ni Afya pia ni ajiira.
Wakizungumza baadhi ya watumishi wajimbo hilo wamesma pamoja na kwamba ni watumishi wa serikali lakini bado ni wakulima kutokan na hali hiyo mbengu zikojuu sana ukilinganisha na beiza mazao zilizopo hali inyo katisha tamaa.
Pia wamesema kuwa watumishi wangazi za chini kuonekana kama hawafai wakati wanapo kuwa wametekeleza majikumu ya uongozi .
Watumishi hao wamesema kumekuwa na tabia ambayo siyo nzuri pale ambapo mtumishi amejenga nyumba au kununua chombo cha usafiri jamii kuona kama mtu huyo kaiibia Serikali sasa wamitumishi hawa watafanya vipi maendeleo yao binafsi kama hawatakuwa na mali zao binafsi.
Aidha wamesema kuwa katika Shule kuna mabomba ya Maji ambapo Mabomba hayo hudaiwa kulipiwa kwa kiwango cha Maji yanayokuwa yametumika hali inayo kuwa ngumu kutokana na kiwango kikubwa kinacho kuwa kinadaiwa pia kutukuwepo kabisa kwa huduma ya Maji kwa baadhi Shule hali inayo pelekea Watoto kutembea umbali mrefu kutafa Maji .
Akijibu maswali Geofrey pinda amesema changamoto za maji na barabara ni maswala ambayo yako katika utekelezaji kwani mpaka sasa kuna matengenezo yanaendele .
Pia amesema ziwa Rukwa niziwa pekee lenye madini Helium amboyo hayapatikani kwingine Duniani kote Zaidi ya Tanzania na Marekani hivyo barabara lazima ziboreshwe ilikuwezakupitika kutokana na uchimbaji utakaokuwepo.
Hata hivyo amezitaka Serikali za Vijiji kutazama namna ambayo itafanya ilikuweza kulekebisha malipo ya Maji mashuleni ilikuweza kuepukana na changamoto za ulipaji.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa