Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkaoni Katavi likiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Majid Mwanga ,Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Silas Ilumba ,Mkurungenzi Mtendaji Bi. Shamim Mwariko na Wakuu wa Divisheni na Vitengo wamefanya ziara ya kutembelea na kujifunza namna hewa ukaa inavyo zarishwa kutokana na misitu ya asili au yakupandwa katika Halmashauri ya Tanganyika inayotekeleza Mradi huo.
Wakiwa katika ziara hiyo ya siku mbili Mtendaji wa kijiji cha Mpembe kata ya katuma Herieth Festo Malekela amesema ili kuweza kufanikisha zoezi la uhifadhi hewa ya ukaa ushirikishwaji wa jamii unahitajika kwani jamii lazima ipate uelewa wa umhimu wa uhifadhi wa Mazingira kwa kuzarisha Hewa ya Ukaa.
Aidha amesema ili kuweza kuepusha changamoto za shughuli za kibinadamu katika maeneo maeneo ambayo ni yauhifadhi wa wa misitu kwa ajili ya hewa ukaa lazima kuwe na maeneo tengefu kwa ajili ya shughuli za kilimo, na ufungaji katika maeneo hayo.
Herieth ameeleza kuwa wameweza kupata faida kutokana na uzarishaji wa Hewa Ukaa kwa kujenga Zahanati, kujenga nyumba za watumishi wa Afya kulipata mishahara ya watumishi, kuwakatia BIMA baadhi ya wanakijiji na kutoa chakula kwa wanafunzi Shuleni.
Naye Kaimu Mkurungenzi Mtendaji wa Tanganyika Alex Mlema amesema kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Halmashauri ya Mpimbwe na Tanganyika endapo Halmashauri ya Mpimbwe itakuwa tayari kuzarisha Hewa ukaa wako tayari kutoa ushirikiano ili kuweza kukamilisha michakato huo.
Kwa upande wake Mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Mwariko amewataka waheshimiwa madiwani na kila kiongozi wa serikali kwanafasi yake kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili kuweza kutumia fursa ya mlima wa lyamba lya mfipa na eneo la WMA ambalo lipo katika eneo la kibaoni na kuhakikisha wanatumia vizuri elimu walioipata Tanganyika.
Mkuu wa Wilaya Mhe.Majid Mwanga naye amesema kuwa kutokana na ziara hiyo nivyema kuonesha ushikamano katika swala hili ili kusiwepo mtu wa kuwa kinyume na wengine kwani uhifadhi wa hewa ukaa unafaida kubwa katika jamii.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa