Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Bi. Shamim Mwariko,leo tarehe 12/02/2025, alizindua mafunzo kwa watendaji wa kata na vijiji pamojana maafisa maendeleo ya jamii kuhusu uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Mafunzohayo yamehudhuriwa na Afisa Maendeleo Mkoa wa Katavi na Mratibu wa Jukwaa laWanawake Mkoa wa Katavi, Ndugu Kennedy, pamoja na Mkuu wa Idara ya Maendeleo yaJamii wa Halmashauri ya Mpimbwe, Ndugu Bernad Lusomyo.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji alisisitiza kuwa ni muhimukuendelea kuboresha na kuimarisha majukwaa ya uwezeshaji wanawake katika kilakata ili kukabiliana na changamoto zinazozikumba maeneo husika. Alisisitiza piaumuhimu wa ushirikiano kati ya watendaji na Jeshi la Polisi ili kukomeshavitendo vya wizi vinavyotokea katika baadhi ya maeneo.
Aidha, Bi. Mwariko aliongeza kuwa ni muhimu kujikinga na magonjwa kamakipindupindu kwa kushirikiana na vituo vya afya na kwa kuhakikisha tunatumiamaji safi na salama. Alisisitiza pia umuhimu wa vyoo bora katika kila kaya nakuwataka kamati za mazingira kuchukua hatua kwa wale wote ambao hawana vyoo,kwa kuanzisha adhabu kama vile faini kwa makosa hayo.
Mkurugenzi Mtendaji pia alizungumzia kuhusu mikopo ya halmashauri ya 10% nakuwataka viongozi wa vikundi vilivyopata mikopo hiyo kuhakikisha wanarejeshamikopo kwa wakati. Aliwataka pia kuhakikisha kuwa wanahakiki watu wanaopatamikopo hiyo kuwa ni wale kutoka maeneo husika, ili iweze kusaidia vikundivingine kupata mikopo kwa urahisi.
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo Mkoa wa Katavi, ambaye pia ni muwezeshajiwa mafunzo haya, alitoa elimu kwa watendaji wa kata na vijiji kuhusu umuhimu wakukuza nguvu za jukwaa la uwezeshaji wanawake katika maeneo ya vijiji na kata.Alisema kuwa muongozo wa jukwaa umeboreshwa kutoka muongozo wa usimamizi wawanawake kiuchumi na sasa umejikita zaidi katika uratibu wa jukwaa lauwezeshaji wanawake kiuchumi, jambo ambalo litasaidia kuimarisha utendaji nakufikia malengo.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa