Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla Pichani akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya Halmashauri kwa Naibu waziri wa Sheria na Katiba Mh.Geofrey Pinda leo tarehe 31 Dec. 2020. Aidha Bi.Mashalla alifanya utambulisho wa Wadau wote waliohudhuria kikao kazi hicho ambao ni Wah. Madiwani wa jimbo la Kavuu, TANESCO,TARURA, Idara ya Maji, Wakuu wa idara na Vitengo, Watendaji wa Kata,Waratibu elimu kata,Wakuu wa shule na Walimu wakuu wote na Watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Bi.Mashalla alitumia fursa hiyo kumpongeza Mh. Naibu waziri kwa ushindi mkubwa wa kishindo alioupata yeye binafsi na chama chake cha (CCM) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 2020, pia kwa kuaminiwa na Mh.Rais Dr.John Joseph Magufuli hata akamteua kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.
Aidha Bi Mashalla alimuomba Mh.Naibu waziri awe huru kusema chochote ambacho anadhani kitasaidia kuitoa Mpimbwe hapa ilipo na kwenda juu zaidi katka maendeleo ya Mpimbwe na Jimbo la Kavuu kwa ujumla wake.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa