Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla Pichani akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Mh. Comrade Juma Homera kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za Wakuu wa Idara.
Aidha Bi.Mashalla amesema kuwa Halmashauri imeongeza idadi ya nyumba hizo kutoka 9 mpaka 10 kwa bajeti ileile.
Pia alimuomba Mh. Mkuu wa Mkoa asaidie uingizaji wa umeme kwa haraka katika mtambo wa kusukuma maji kuelekea eneo la ujenzi wa nyumba hizo ili kupunguza gharama za kutumia mafuta kuendeshea mtambo huo wa kusukuma maji
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa