Mafunzo juu ya anwani Za Makazi na postikodi yametolewa kwa Watendaji wa Waijiji, Wenyeviti wa vijiji, Maborozi wa Mitaa, na watendaji wa kata Yametolewa leo tarehe 14/02/2022 katika kata ya Usevya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe
Mafunzo hayo yaliyo hudhuriwa na Diwani wa kata ya Usevya, Afisa tarafa wa Usevya na wajumbe Wengine yametolewa na Kamati ya anwani ya Makazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Aidha mratibu wa anwani za makazi ameeleza juu ya umhimu wa anwani za makazi na postikodi ambapo amesema itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali , za kijamii na bidhaa kuwafikia wanachi kwa urahisi sambamba na kupunguza muda mwingi uliokuwa unatumika awali kupata huduma, manufaa mengine ya anwani za makazi ni kutoa fursa ya ajira kwa vijana, ulinzi na usalama, kuongeza pato la nchi, kuharakisha utafiti na kiogeza utalii,hivyo ameomba viongozi waliopatiwa mafunzo kuhamasisha wananchi kushiriki katika kujiwekea wenyewe miundombinu ya anwani za makazi ambapo itaipunguzia serilikali gharama.
Na Odetha Salum
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa