Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa katavi limeeleza kilio cha wakulima kutokuwa na elimu ya matumizi ya pembejeo za kilimo hususani mbolea zinazotumika katika kilimo na kuuzwa bei kubwa isiyo ya Serikali.
Wakichangia hoja katika kikao cha baraza hilo la kupitia taarifa ya robo ya pili wamesema baadhi ya maduka yanayotoa huduma yakuuza pembejeo za kilimo wamekuwa hawatoi elimu yanamna bora ya kutumia pembejeo hizi hali inayo pelekea wakulima kuhalibikiwa mazao kwa kushinda kutofautisha matumizi ya mbole.
Aidha baraza hilo limebainisha kuwa serikali ilitoa usafili wa pikiki kwa ajili ya kurahisisha usafili kwa maafisa ugani ili kuweza kuwafikia wakulima kwa urahisi lakini maafisa hao hawafanyi hivyo badala yake wakulima kutumia uelewa wao kulima mazao yao
akifafanua juu ya hoja hizo Afisa kilimo wa Halmashauri ya Mpimbwe George Magile amesema wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kwa wauzaji wapembejeo za kilimo kwa kuwaandikia barua na kuwataka watoa huduma wawe watu wenye weredi mkubwa
katika maswala ya kilimo ili waweze kutoa ushauri unaostahili kwa wakulima.
Pia amesema Maafisa ugani kwa mjibu wa Sheria wanatakiwa kuhudumia wakulima sita kila siku katika maeneo yao .
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa