Katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya sita inayo ongozwa na mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani mwezi machi, 2021hadi machi, 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe imepokea jumla ya Tsh.Bilioni 10,215,219,920.34 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo .
Akisoma Taarifa utekelezaji Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi . Catherine Mashalla Amesema hayo Katika kongamano la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa katavi.
Bi.Catherine Mashalla amesema katika Sekta ya Afya jumla ya Tsh 4,641,041,961.8 zimewezesha kujenga Majengo 9 ya Hospitali ya Wilaya pamoja na nyumba ya Watumishi , Ujenzi wa Vituo 3 vya Afya, Ujenzi wa zahanati 5, Ununuzi wa Vifaa Tiba kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za Afya , utoaji wa Hamasa ya Maswala ya Lishe , utoaji wa huduma za chanjo ikiwemo polio, Surua, na UVIKO19.
Katika Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari Serikali imetoa jumla ya Tsh. 3,069,035,000.00
Ambazo zimetumika katika ujenzi na ukamilishaji wa Miundombinu mbalimbali katika Shule ya msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na ujenzi wa matundu wa vyoo , utengenezaji wa madawati kwa shule za Msingi , utengenezaji wa viti na meza kwa shule za Sekondari , Ujenzi wa Nyumba za Walimu , ukarabati wa Mabweni pamoja na ukamilishaji wa Maabara.
Sanjali na hayo amesema Serikali imewezesha Tsh. 393,735,062.59 ya mikopo ya Vikundi vya Wanawake , Vijana , na Watu Wenye Ulemavu kwenye ununuzi wa mashine za kukamua mafuta ya alizeti, mashine ya kutengeneza Tofali za Block, Guta za kubeba Mizingo, Pikipiki Pamoja na huduma nyingine za Ujasiliamali
Jumla ya 3,937,395,947.90 zimekusanywa ndani ya miaka Miwili kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya Mapato ya Ndani.
Amesema pia jumla ya Watumishi 139 ajira mpya wameajiriwa katika Halmashauri ya Mpimbwe na watumishi 318 walipandishwa vyeo na nyumba 19 za watumishi kujengwa zilizo gharimu jumla ya fedha kiasi cha Tsh.1, 240, 000,000. 00 ambazo zimerahisisha utendaji kazi kwa watumishi na kuwawekea Mazingira mazuri ya kiutendaji.
Bi. Mashalla amesema katika swala zima la uhifadhi wa mazingira Serikali imetoa Tsh. 153,053,069.62. ambayo itasaidia katika utunzaji wa Mazingira katika Halmashauri ya Mpimbwe ikiwa ni pamoja na kulinda maeneo tengefu, Vyanzo vya maji na Uhifadhi wa uoto.
Aidha amesema katika Sekta ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi sh. 91,352,650.00
zimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa skimu ya umwagilia kilida , Mbolea ya Ruzuku , Ukarabati wa Machinjio na ujenzi wa majosho. Aidha, Serikali imetoa Tsh. 627, 002,176.98 kwa ajili ya shughuli Sensa ya Watu na Makazi,
Kwaupande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Majid Mwanga ametoa pongezi nyingi kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia suluhu hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Miundo mbinu katika Wilaya ya Mlele pia amewataka wananchi kuendelea kuitunza Miradi na kuepukana na uharibifu unaojitokeza katika Miundombinu inayo wekwa na Serikali.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa