Mwenyekiti wa kamati ya Siasa Mkoa wa Katavi Mhe. Iddy Kimanta akimbatana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko wametembelea na kukagua Miradi ya Maendelea katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe.
Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Iddy Kimanta amewataka wakurungenzi kuhakikisha wanasimamia miradi yote inayo endelea katika Halamashauri ili kuweza kukamilika kwa wakati uliokusudiwa na kuwa chachu kwa wananchi.
Aidha amesema katika miradi ya Elimu yote kufika januari 4 madarasa yote yaweyamekamilika kwa kuwekwa thamani zote zinazotakiwa ili wanafunzi watakapokuwa wameripoti wakute kila kitu kiko tayari.
Pia amesisitza kuongeza usimamizi wa kutosha katika miradi yote ili iweze kujengwa katika ubora unao takiwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameahidi kuhakikisha usimamizi wa mradi yote inayo endelea katika Mkoa wa katavi kukamilika kwa wakati ikiwa nipamoja na kuimarisha usimamizi wa miradi hiyo.
Mkuu wa mkoa ametumia nafasi hiyo kuwataka wazazi wote kuhakiksha wanawaandikisha watoto wote wanaotakiwa kuanza Darasa la awali waandikishwe mapema kabla ya kufika mwenzi wa kwanza pia na wale wanao tarajia kuanza kidato cha kwanza wote kuripoti shule zitakapokuwa zimefunguliwa.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa