Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh. Majid Mwanga amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kwa ajili ya kutembelea , kusikiliza , kutatua kero za Wananchi na kuhamasisha wananchi kuhakikisha watoto wote wenye umri chini ya miaka nane kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa polio ili kuweza kuepuka madhara yatokanayo na ugonjwa huo.
Akiwa katika kata ya Mbede , Usevya Ikuba,Majimoto , kibaoni , Mwamapuli, na Chamalendi katika ziara hiyo Mhe Majid Mwanga amebaini changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi katika maeneo yao ambayo wanaishi licha ya kuwepo kwa viongozi ambao wanatakiwa kuwazipatia ufumbuzi na badala yake wengine kuwa sehemu ya kuzalisha changamoto.
Aidha amebaini kuwa Pamoja na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi bado baadhi ya viongozi wa kata wamekuwa wakiendelea kuchangisha wananchi michango ambayo ni kinyume na utaratibu
Kutokana na hali hii Mkuu wa Wilaya amemuelekeza Mkurugenzi mtendaji kuwachukulia hatua za kinidhamu Mtendaji wa kijiji pamoja na mtendaji wa kata ya Ikuba kwa kuchangisha michango wananchi
Katika ziara hiyo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kuwachukulia hatua vijana ambao wanajiita changulaga ambao wanafanya uzalilishaji kwa watoto wa kike.
Pia amewataka wananchi kuendelea kujiandikisha katika daftari ili kupata mbolea za ruzuku zilizotolewa na Mhe .Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani..
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa