Kufuatia Mlipuko wa ugonjwa wa Surua uliojitokeza katika Halmashauri ya Mpimbwe Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Majid Mwanga amefanya ziara ya siku Nne katika kata za Usevya, Ikuba , Mbede, Mwamapuli, Mamba , Majimoto, Kibaoni Chamalendi na Kasansa ilikutoa elimu juu ya mripuko wa ugonjwa wa Surua.
Akiambatana na katamati ya ulizi na Usalama Mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya mpimbwe pamoja na mganga mkuu wa Halmashauri hiyo hapo jana tarehe 20 .02.2023 amesema idadi ya wagonjwa imeongezeka kufikia 840 huku kati ya wagonjwa hao wengine wakiwa wamesha pona na vifo vikisalia kuwa 12.
Kwa upande wake Mganga mkuu Martin Lohay amesema idadi hii inaongezeka kutokana na kuwepo kwa watoto wengi ambao wazazi wao hawakuzingatia huduma ya chanjo hivyo kusababisha mripuko huu kuendelea kujitokeza.
Hivyo amewataka wananchi kumuwahisha mgonjwa kituo cha afya mala tu wanapoona dalili za ugonjwa huo ilikuepusha madhara zaidi.
Aidha Mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Bi Catherine Mashalla Amewataka wananchi kuendelea kuwapeleka watoto kupata chanjo.
Mwisho
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa