Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Majid Hemed Mwanga akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na kaimu Mkurugezi Martin Lohay wametembelea katika kaya 51 zilizopo katika kata ya Majimoto, zilizokumbwa na upepo kutokana na mvua kubwa kunyesha na kusababisha Uharibifu wa makazi .
Akitoa pole kwa wahanga hao katika kata hiyo amemtaka Mratibu wa Maafa wa Halmashauri ya Mpimbwe ndg Saak Muok kufanya tathimini ya haraka ilikuweza kupata ufumbuzi wa changamoto zilizojitokeza wakati wa Mvua hiyo .
Kwa upande wake Editha Swima mama wawatoto watatu Mkazi wa kijiji cha Namanyere ambaye ni mhanga amesema mvua hiyo iliyo ambatana na upepo mkali ilitokea majira ya mchana ambapo mvua Hiyo iliangusha nyumba pamoja na tofali kutoka Juu lili mwangukia yeye na Mwanaye Catherine na kusababisha kuumia sehemu ya mguuni ikiwa ni pamoja na kuharibu chakula chote cha hakiba walichokuwa wamekihifadhi ndani.
Aidha amesema kwa sasa amesaidiwa na Majirani ambao wamempa hifadhi ya Muda hivyo amiomba Serikali kumsaidia iliaweze kupata pakuishi.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa