MALENGO
Kupitia uhalali na usahihi wa taarifa za Fedha na utendaji wake,na namna taarifa hizo zilivyopatikana;
a) Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti wa makusanyo utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha za Halmashauri.
b) Kupitia na kutoa taarifa juu ya kufuatwa kwa taratibu za fedha zilizowekwa, sheria maagizo na taratibu za kihasibu zinazotolewa na Waziri katika nyakati mbalimbali ili kuwepo kwa matumizi mazuri ya fedha.
c) Kupitia na kutoa taarifa juu ya usahihi wa mpangilio na mgawanyo wa mapato na matumizi ya akaunti.
d) Kupitia na kutoa taarifa juu ya usahihi na uaminifu wa takwimu za fedha zilizotumika katika kuandaa taarifa za fedha na taarifa nyingine.
e) Kupitia na kutoa taarifa juu ya mifumo iliyopo inayotumika kutunza mali.
Mkaguzi wa ndani anapaswa kuhakiki na kutathmini taarifa za mwisho za Fedha ,kupima mfumo wa udhibiti wa Fedha ufanisi wake katika Fedha za umma kama ilivyoainishwa katika muongozo wa taaluma wa kimataifa(IPPF) ,fungu namba 2130 la ukaguzi wa ndani kwa kupitia yafuatayo:
a) Mfumo wa udhibiti wa ndani.
b) Uwasilishwaji wa taarifa zote za Fedha
c) Utoaji wa taarifa za Fedha unakidhi misingi ya uhasibu
d) Uthibitisho wa rasimali na madeni ya halmashauri unaambatana na ushaidi wa nyaraka.
e) Rasilimali,madeni,mapato na matumizi yanawasishwa kwa ushihi kwenye taarifa za Fedha
f) Rasilimali na madeni yaliyoripotiwa yanamilikiwa na halmashauri
g) Ukamilifu wa taarifa za Fedha za halmashauri wa kipindi husika
h) Usahihi wa upimaji na tathmini ya taarifa za rasilimali,madeni,mapato na matumizi
i) Uhakiki wa nyaraka za Fedha.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa